Wabunge nchini Afrika Kusini, wamepiga kura inayopendekeza kufungwa kwa ubalozi wa Israeli mjini Pretoria pamoja na kusitishwa kwa uhusiano wowote wa kidiplomasia kati ya nchi hizo mbili.
Chama tawala cha ANC ambacho kina uwakilishwaji mkubwa kwenye bunge, kimekuwa kikiituhumu Israeli kuhsiana na oparesheni zake katika ukanda wa Gaza na kimeunga mkono muswada huo kwenye bunge.
Wabunge wamesema wamepitisha muswada huo unaoruhusu kufungwa kwa ubalozi wa Israeli na kusitishwa kwa uhusiano wa kidplomasia hadi pale Israeli itakapokubali kusitishwa kwa mapigano na kuruhusu mazunguzmo yenye tija.
Muswada huo uliuungwa mkono na wabunge 248 dhidi ya 91.
Kuelekea upigaji kura kuhusiana na muswada huo, Israeli ilimuita nyumbani balozi wake kwa majadiliano, hatua ambayo ilisema imetokana na matamshi ya taifa hilo la Afrika.
Hivi karibuni, rais Cyril Ramaphosa alisema nchi ya Israeli inafaa kuwajibishwa katika mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita ya ICC kutokana na kile alichosema ni ukiukaji wa haki za binadamu. Afrika Kusini pia ilimwagiza balozi wake nchini Israeli kurejea nyumbani.