Baada ya South Africa kusema kuwa Media za Nyumbani zitaplay muziki wa nyumbani kwa asilimia 90, msanii toka Label ya WCB Diamond Platnumz amefunga mawazo yake.
Akizungumza na Ayo TV staa huyo alisema…‘Wasanii wanatakiwa kutengeneza nyimbo kali ili media mbalimbali ziweze kuacha kucheza nyimbo za nje, kwa mfano zamani tulikuwa tukitoa baadhi ya video zinakubalika lakini sio kama video za nchi jirani lakini tulivyoanza kushoot video nzuri wenyewe wanaamini kuwa video za vijana wao ni kali’- Diamond Platnumz
‘Tukumbuke zamani watu walikuwa wanapenda sana movie za nchi za nje za kutoka East Africa, Nigeria na nchi zingine lakini walivyoanza wakina marehemu Kanumba, Ray kutengeneza movie soko lilikufa la watu wa nchi za nje tulikuwa tunapenda movie za kitanzania kwahiyo nasema tuache kulalamika tutengeneze kitu ambacho ni kizuri na kitapendwa zaidi kuliko kile cha nchi jirani’- Diamond Platnumz
ULIIKOSA HII YA DIAMOND KUHUSU NI MASWALI GANI AMBAYO HATAKI KUULIZWA MWAKA 2016 BASI ITAZAME HII VIDEO HAPA
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE