Arnold Schwarzenegger alizuiliwa kwa muda katika Uwanja wa Ndege wa Munich kwa kushindwa kutaja thamani ya saa ya kifahari aliyoleta kutokea Marekani.
Muigizaji huyo na gavana wa zamani wa California alizuiliwa na mawakala wa forodha alipowasili Munich siku ya Jumatano (17 Januari), na alicheleweshwa kwa saa tatu huku kukowa na uchunguzi wa madai ya kukwepa kulipa ushuru ulianzishwa kwa sababu saa hiyo ilidhamiriwa kuuzwa ndani ya Umoja wa Ulaya.
Shirika lisilo la faida la muigizaji huyo mwenye umri wa miaka 76, Schwarzenegger Climate Initiative, liliambia shirika la habari la Ujerumani DPA kwamba mwigizaji huyo alipanga kuuza saa hiyo, ambayo ina picha ya Schwarzenegger kama The Terminator nyuma, katika mnada huko Kitzbuhel, Austria takriban kilomita 89 kutoka Munich, ili kufaidi mipango ya hali ya hewa.
Kulingana na vyombo vya habari vya nchi hiyo, saa hiyo imetengenezwa maalum na mtengenezaji wa saa za kifahari Audemars Piguet na inatarajiwa kupigwa mnada kwa angalau $50,000 (€46,000).
Wakati wa kuzuiliwa kwa muigizaji huyo kwa saa tatu, msemaji wa forodha wa Munich aliiambia DPA: “Ikiwa bidhaa zitasalia katika EU, unapaswa kulipa kodi na ushuru. Hiyo inatumika kwa kila mtu.”
Muigizaji huyo aliruhusiwa kuchukua saa pamoja naye, na BILD iliripoti kwamba alipaswa kulipa faini ya maelfu kadhaa ya euro kuondoka.