Makamu wa Rais wa Zimbabwe, Kembo Mohadi amejiuzulu kwa madai ya kulinda taswira nzuri ya serikali kufuatia ripoti za vyombo vya habari nchini humo kudai kuwa kiongozi huyo amekuwa na mwenendo usiofaa.
Mohadi amesema amefikia uamuzi huo “sio kama woga bali ni ishara ya kuonyesha heshima kubwa kwa ofisi ya rais.”
Wiki mbili zilizopita mtandao wa habari ‘ZimLive’ uliripoti kuwa Mohadi alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na wanawake walioolewa pamoja na mmoja wa watumishi wake kitendo kilichotafsiriwa kuwa ni ukosefu wa nidhabu kwa kiongozi huyo wa juu.
Mohadi alikataa mashtaka hayo wiki iliyopita akisema kuwa atatafuta njia ya kisheria.
EXCLUSIVE: MAAJABU YA MTOTO GENIUS WA HESABU, “SIJAFUNDISHWA, WAKUBWA HAWANIWEZI”