Mtu wangu hii ni stori ambayo bila shaka itakugusa na hasa kama unamiliki simu ya Smartphone, suala la kuishiwa chaji kila mara au katikati ya siku na bahati mbaya ikatokea umesahau charger yako limekua ni kawaida sana kwa watumiaji wa Smartphone. Leo nakuletea sababu sita za kwanini betri ya simu yako huisha au kufa mapema tofauti na maelekezo ya watengenezaji wa simu.
1. KUCHAJI SIMU MPAKA 100%
Watafiti wanashauri matumizi ya simu yako yasizidi mpaka ikashuka chini ya asilimia 30 kwasababu uimara wa berti yako upo kwenye asilimia kati ya 30 mpaka 80, hivyo unatakiwa kuichaji simu yako kabla haijazima kabisa na wakati wa kuchaji hutakiwi kuitumia kabla haijafikisha asilimia 80 ya kiwango cha chaji tangu ulipoiweka kwenye umeme.
2. KUTUMIA SIMU MPAKA CHAJI INAISHA
Kila unapotumia simu yako mpaka chaji inaisha kabisa na kuzima, tambua kuwa unazidi kuipa ubovu betri yako, na kuifanya iwe dhaifu kila mara. Ukiona simu yako imepungua chaji mpaka asilimia 10% hiyo ni hatari, anza kutafuta charger haraka!
3. SIMU KUCHEMKA
Tatizo hili linawakuta watu wengi na wengi wao hudhani ni jambo la kawaida tu, lakini inaelezwa kuwa ni moja kati ya sababu zinazoua uwezo wa simu kukaa na chaji kwa muda mrefu, pia huharibu mfumo wa umeme ndani ya simu yako. Simu za iPhone mara nyingi huonesha alama ya kukuonya kuwa simu imechemka; hivyo ukiona alama hiyo kwenye simu yako unatakiwa kuizima hata kwa dakika 5 kisha iwashe!
4. KUCHAJI KWA KUTUMIA USB
Hili imekua jambo la kawaida sana siku hizi, watumiaji wengi wa simu hawatumii chrger kamili za simu zao na badala yake hutumia zaidi USB kama njia ya kuchaji simu, na hii ni kutona mazingira ya kupata soketi za umeme au tu kuwa karibu na simu huku ikiwa imechomekwa kwenye Laptop. Kutumia USB kuchaji simu kila mara kunaipa ubovu betri yako na kusababisha ife mapema. USB hazipitishi umeme sawa na charger kamili za simu.
5. KUIACHA SIMU ICHAJI ZAIDI YA MUDA WA KAWAIDA
Kama unatumia bidhaa za Apple basi jambo hili halikupi shida, lakini kama uko na bidhaa za Android suala la kuchaji simu yako kwa umakini inabidi lipewe kipaumbele sana. Unatakiwa kuiangalia simu yako mara kwa mara ili isichaji mpaka asilimia 100 na ikaendelea kubaki kwenye umeme mtu wangu.
6. KUCHAJI SIMU IKIWA KWENYE KAVA
Ukiona simu yako inapata joto zaidi ya hali ya kawaida, hakikisha unaondoa kava ya nje ili kupunguza ongezeko la joto simu ikiwa chaji. Kumbuka joto linalozidi huathiri kwa kiasi kikubwa uimara wa betri ya simu yako.
ULIPITWA NA TAARIFA YA AJALI YA BASI LA NEW FORCE ILIYOTOKEA MKOANI NJOMBE? ISIKILIZE HAPA