Mkuu wa Wilaya ya Hai Lengai Ole Sabaya amemuweka ndani Mtumishi wa Serikali katika Manispa ya Moshi kwa tuhuma za kujihusisha na utapeli.
DC Sabaya amesema uamuzi huo umetokana na madai ya Walimu wapatao tisa kulalamika kutapeliwa na Taasisi inayojihusisha na biashara mtandaoni.
Mtuhumiwa aliyekamatwa kwa ajili ya kuhojiwa na Polisi pamoja na TAKUKURU ametajwa kuwa ni mtumishi wa Halmashauri ya Manispaa ya Moshi, ambaye alifanya ushawishi kwa Walimu Wilayani Hai, ambao waliingiza fedha kwenye Taasisi hiyo kati ya Tsh. Milioni 3 hadi Milioni 4.2.