Mkuu wa Wilaya ya Hai Lengai Ole Sabaya ameagiza kukamatwa kwa Afisa Uhusiano wa Kampuni ya Michiru baada ya kutuhumiwa na Wafanyakazi wenzake kuwanyanyasa kingono na kuwachonganisha na Viongozi pamoja na baadhi ya wanaume kulalamika kuchukuliwa kwa wanawake zao.
Akizungumza baada ya kutoa maagizo hayo DC Sabaya amesema haiwezekani alalamikiwe na Wanawake 22 kuhusu tuhuma za ngono “Watu 22 wanawezaje kukutuhumu mtu mmoja kwamba anatutaka kimapenzi na wameandika barua”.