Mkurugenzi wa Mashtaka Nchini (DPP) Silvester Mwakitalu, leo May 05,2024 amewasilisha katika Mahakama Kuu ya Tanzania masijala ya Arusha ombi la kuiondoa rufaa No.155 ya Mwaka 2022 aliyokuwa ameikata dhidi ya Aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai Lengai Ole Sabaya na wenzake saba ya kudaiwa kujipatia Tsh. milioni 90 kwa Mfanyabiashara Francis Mroso.
Rufaa hiyo ilikatwa na Jamhuri baada ya Sabaya na wenzake kushinda kesi hiyo ya Uhujumu uchumi No.27 ya mwaka 2021 katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Arusha iliyosikilizwa na kuamuliwa na Hakimu Patricia Kisinda.
Wakili wa Sabaya Moses Mahuna amesema Sabaya hana lengo la kudai fidia na kilichofutwa ni rufaa iliyotokana na kesi na kwa sasa yupo huru na hana kesi yeyote na kwamba kwa mujibu wa Mahakama yenyewe Sabaya kwa sasa hana rekodi yoyote ya uhalifu na hana shauri lingine lolote katika chombo chochote cha sheria na kumfanya kumalizana rasmi na Mahakama.