Si jambo la kawaida kuona watu wakisafirishwa kwa kutumia usafiri wa Guta ama toroli lakini hilo limewezekana jijini Dar es Salaam maeneo ya Jangwani ambapo kutokana na mafuriko iliwabidi watu wavushwe kwa kutumia usafiri huo.
Hatua hiyo inatokana na mvua zinazoendelea kunyesha jijini Dar es Salaam, ambapo Ayo Tv na Millardayo.com ilifika eneo la Jangwani na kushudia changamoto ya usafiri ambapo ilisababisha watu wabebwe kwa kutumia Guta ama Toroli.