Kesi inayowakabili washtakiwa watatu akiwemo Mbunge wa Mbozi Pascal Haonga ambao wanadaiwa kuwazuia Askari Polisi kutekeleza majukumu yao , kufanya vurugu kwenye uchaguzi wa mamlaka ya mji mdogo na kukataa kutoka nje ya ukumbi imeahirishwa hadi August 10, 2018.
Imedaiwa na upande wa mashtaka kwa pamoja waliwazuia Polisi kutekeleza majukumu yao , kufanya vurugu na kukataa kutoka nje ya ukumbi. Akiahirisha kesi hiyo Hakimu Mfawidhi Nemes Chami amesema ameshindwa kutoa hukumu kutokana na majukumu mengi ya kimahakama pia uzito wa kesi yenyewe.
Nje ya Mahakama Wakili Boniphace Mwabukusi amesema anaunga mkono uamuzi wa Mahakama ili kutenda haki kwa pande zote mbili. Naye Mbunge wa Tunduma Frank Mwakajoka amesema Mahakama ndiyo chombo huru ana imani itatenda haki.
RC Makalla asubirisha zoezi la Machinga kupewa Vitambulisho na TRA