Ni headline kutokea Bungeni Dodoma wakati Wabunge walikuwa wakichangia mapendekezo yao katika bajeti ya Waziri Mkuu kwa mwaka wa fedha 2018/19 ambapo Mbunge wa viti maalum CCM Hawa Mchafu Chakoma ambaye ameishauri serikali kuanzisha namna bora ya kuanziasha mpango wa pensheni kwa wazee waliolitumikia taifa.
Hawa Mchafu amesema…>>>“Nashindwa kufahamu mfuko wa moja kwa moja ambao upo kwa ajili ya wazee, muda umefika sasa ule mchakato wa pensheni kwa wazee uje sasa ili kuweza kuwasaidia wazee wa taifa letu ambao kwa nafasi zao walisaidia sana nchi yetu”
“Niipongeze Serikali pia kwa kuanzisha miradi mbalimbali mikubwa ikiwemo ujenzi wa bomba la mafuta, ujenzi wa viwanja vya ndege n.k ni wazi itaambatana na upatikanaji wa ajira lakini niishauri Serikali ihakikishe inafuatilia mikataba ya kazi kwa watanzania inayofanyika katika miradi hiyo kwamaana kumekuwa na ukakasi mkubwa sana mikataba mingi inaukiukwaji wa kisheria” –Hawa Mchafu
Rais Magufuli alivyokabidhi Toyota Land Cruiser mpyaa aliyoahidi