Waziri wa Fedha wa Kenya, Ukur Yatani, amepinga ripoti zinazoashiria kwamba bandari kuu ya nchini Kenya huenda ikachukuliwa na China ikiwa itashindwa kulipa mikopo mikubwa iliyopewa kufadhili ujenzi wa reli mpya.
Gharama ya ujenzi wa reli hiyo mpya ya urefu wa kilo mita 472 ni karibia mara tatu ya viwango vya kimataifa ikilinganishwa na na makadirio ya awali.
Jana Jumatatu gazeti moja liliripoti kuwa China huenda ikachukua usimamizi wa bandari ya Mombasa ikiwa Kenya itashindwa kulipa mkopo wa dola bilioni 3.2 sawa na (£2.3bn) .
Lakini katika taarifa ya waziri wa fedha alisema: “Hakuna hatari kabisa ya China au nchi nyingine yoyote kuchukua bandari hiyo,” amesema.
Aliongeza kuwa mkopo wa ujenzi wa reli hauwezi: “Kulipwa kupitia mfuko mwingine wowote au chombo kingine chochote bila idhini ya bunge.
“Serikali ya Kenya haiwezi na haijaahidi kutoa mali ya umma kama dhamana ya kulipa deni kwa sababu hatua kama hiyo … inakiuka masharti ya makubaliano yake ya mikopo iliyopo,” Yatani.