Ametoa agizo hilo leo Mei 20, 2021 alipozungumza na Menejementi na Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kwenye Makao Makuu ya Zamani ya Shirika hilo jijini Dar es Salaam.
“Lazima tufundishane kuwa makini, kila siku lazima tukague vifaa vyetu ili huduma ipatikane muda wote, hakuna kuwasimamisha kwa siku 10, wakae pembeni hadi timu inayochunguza itakapotoa matokeo, inawezekana sio wao tu, Waziri endelea na uchunguzi”———Majaliwa
Waziri Mkuu ameliagiza pia Shirika hilo kuhakikisha wanakuwa na mfumo wa dharura ‘backup’ utakaotumika pindi kunapotokea changamoto za kimfumo———-“Mmetengeneza usumbufu mkubwa sana, mlijua lazima kuwe na backup lakini hakuna, toka pale tulipoanza kutoa huduma mpaka leo kwanini hakuna backup, hilo ni jukumu lenu”.