Baada ya video zinazosambaa mtandaoni zikionesha jaribio la utekaji dhidi ya Deogratius Tarimo, Mfanyabiashara na Mkazi wa Kibaha, Mkoani Pwani, sasa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Det Tulia Ackson amejitokeza kukanusha juu ya taarifa zilizodaiwa kuwa miongoni mwa watu waliokuwa wakimkamata Mfanyabiashara huyo kuwa ni msaidizi wake.