amilia ya Marehemu Ally Khalifa Bakari, Mtoto mwenye umri wa miaka tisa ambaye amefariki mara baada ya kupigwa na kitu chenye ncha kali kichwani na mwenzake hadi kupelekea kufariki Dunia, imeiomba Serikali imwachie huru Mtoto mwenye umri wa miaka tisa Mwanafunzi wa Darasa la 3 Shule ya Msingi Kichangani Wilayani Korogwe Mkoani Tanga, ambaye amefanya tukio hilo, Familia hiyo inasema kilichotokea ni makosa ya kibinadamu.
Msemaji wa Familia hiyo Adriano Petro ameiambia Ayo TV na Millardayo.com kuwa ingawa Mtoto wao amefariki kilichotokea ni mapenzi ya Mungu kwakuwa Watoto hao walikuwa wakicheza pamoja siku zote na ikatokea bahati mbaya January 28 mwaka huu wakiwa wanatokea Msikitini njiani wakagombana na kupigana hadi kupelekea Ally kufariki wakati anapelekwa Hospitali.
MKE WA MUUZA MADINI ALIYEUAWA, ASIMULIA KWA UCHUNGU ‘NINA UJAUZITO, WAMEMUUA’