Mapema wiki hii habari iliyokamata headlines ni kuhusu sakata la muigizaji maarufu kutokea nchini Marekani Tyrese Gibson baada ya kuagizwa kulipa takriban dola 650,000 (Tzs Bil 1.527) kama gharama za matunzo ya mtoto na ada za wakili katika kesi ya gharama za matumizi na malezi (child support) ya familia inayomkabili staa huyo.
Mtandao wa TMZ iliripoti kuwa Tyrese alifikishwa katika mahakama ya Kaunti ya Fulton nchini Marekani mapema jana, ambapo jaji aliamua kwamba staa huyo alihitaji kumlipa aliyekuwa mke wake Samantha Lee Gibson $237,944 ambazo ni pesa za kitanzania takriban milioni 559 pamoja na $399,000 (Tzs Mil 937,849,500) kwa wakili wa Samantha.