Wanaharakati wa Haki za Binadamu wamekimbilia Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dar es Salaam kuomba kufungua kesi ya kupinga Tozo mpya za miamala katika simu.
Hatua hiyo inakuja baada ya Serikali ya Tanzania kupitisha Tozo mpya za Miamala katika simu, jambo ambalo limeibua hisia za wengi huku wananchi wakiwa wanalalamikia makato kuwa makubwa.
Odero Charles Odero ni Wakili ambaye pia ni Mwanaharakati wa Haki za Binadamu akiwa miongoni mwa waliowasilisha maombi hayo Mahakama Kuu ya Tanzania.
“Tumeamua kufungua kesi, kuleta maombi Mahakama Kuu ya Tanzania Masjala ya Dar es Salaam kuweza kuomba Mahakama ituruhusu kufungua maombi ya marejeo ya Sheria ili kuweza kupitia sheria ya Fedha ya mwaka 2021/2021 pamoja na Kanuni zake ambazo sheria hizo ilimpa mamlaka Waziri mwenye dhamana Waziri wa Fedha na Mipango kutunga Kanuni ambazo zimezaa Tozo kwenye Miamala ya Simu, binafsi kama Mwanaharakati wa Haki za Binadamu tunaona upitishwaji wa Kanuni hizo haukufuata taratibu,” amesema Odero.
SAKATA LA TOZO ZA SIMU: WANAHARAKATI WAKIMBILIA MAHAKAMANI “WAZIRI, MWANASHERIA MKUU WAMEITWA”
VIDEO MESSI ALIVYOTUA UFARANSA, KUANZA KUICHEZEA “PSG”, MASHABIKI WAJITOKEZA KUMPOKEA