Mohamed Salah si jina maarufu zaidi tna nyuma ya jezi za Liverpool.
Tangu ajiunge na klabu hiyo mwaka 2017 kwa ada iliyoripotiwa kuwa ya pauni milioni 43, Salah amekuwa mtaji wa Liverpool.
Chini ya Jurgen Klopp, Salah pia alikua mmoja wa wachezaji bora zaidi duniani.
Katika kipindi cha miaka miwili iliyopita, Salah alikuwa jina na nambari iliyouzwa zaidi nyuma ya jezi za mashabiki wa Liverpool.
Hata hivyo, kama vile Liverpool walivyofichua 10 bora zaidi, Salah hayupo tena kileleni.
Nafasi ya ‘Mfalme wa Misri’ imechukuliwa na mchezaji aliyesajiliwa na Liverpool majira ya kiangazi Dominik Szoboszlai, ambaye tayari amefanya makubwa miongoni mwa waamini wa Reds.
Kiungo wa kati wa Hungary Szoboszlai alijiunga na Liverpool kutoka klabu ya RB Leipzig ya Ujerumani ya Bundesliga baada ya klabu hiyo ya Anfield kuanzisha kifungu cha pauni milioni 60 cha kutolewa kwenye mkataba wake.
Szoboszlai alifunga bao lake la kwanza kwa The Reds wakati wa ushindi wa 3-1 dhidi ya Aston Villa Uwanja wa Anfield mapema mwezi huu.
Mchezaji mwingine mpya, Alexis Mac Allister aliorodheshwa katika nafasi ya tatu kwenye jezi 10 maarufu zaidi za Liverpool. Huku Trent Alexander-Arnold na Darwin Nunez wakikamilisha tano bora.
Luis Diaz alikuwa wa sita, mlinda mlango Alisson Becker wa saba, nahodha mpya wa klabu Virgil van Dijk wa nane, Cody Gakpo wa tisa na Andy Robertson katika nafasi ya 10.