Klabu ya Liverpool ipo kwenye mzungumzo na nyota wao raia wa Misri Mohamed Salah kwa ajili ya kuongeza mkataba mpya wa kuendelea kusalia Anfield.
Taarifa kutoka Uingereza zinaripoti kuwa mazungumzo hayo yamefikia pazuri na Salah yuko kwenye hatua za mwisho za kusaini mkataba mpya wa kuendelea kusalia klabuni hapo.
Ikumbukwe, kuwa mkataba wa nyota huyo aliyeanza vizuri msimu huu ulikuwa unaelekea ukingoni na hapo awali kulikuwa na taarifa kuwa huwenda angeondoka Liverpool kutokana na ukimya wa klabu hiyo juu ya mazungumzo ya kusaini kandarasi mpya.
Tangu kuanza kwa msimu huu Salah amefunga magoli 13 na kutoa pasi 9 za magoli katika michezo 15 ya Ligi Kuu Uingereza aliyocheza mpaka sasa.