Mbunge wa Jimbo la Mchinga Salma Kikwete ameapa kutounga mkono vitendo vilivyoibuka ambavyo ni kinyume cha tamaduni za Kitanzania vya ukatili kwa Watoto Pamoja na mapenzi ya Jinsia moja.
Kikwete amesema hilo akichangia hoja ya waziri mkuu Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kuhusu mapitio na mwelekeo wa kazi za Serikali na makadirio ya mapato na matumizi ya fedha za ofisi ya Waziri Mkuu na Ofisi ya Bunge kwa mwaka 2023/2024.
“Hili jambo nilakulaaniwa na sisi wabunge tuwe na azimio la kulikataa hili jambo leo kwenye hii dunia kuwa watu wameitengeneza utaratibu wa kutengeneza watoto wawili sisi tulikuwa tunazaa Watoto wengi dunia hii hii wanatuletea ndoa za jinsia moja hivi tutakuwa na kizazi sisi mwanaume akifanyiwa vitendo vile hawezi kufanyakazi atapata wapi watoto” Mbunge Salma Kikwete