Bado ni headlines za mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania anayekipiga katika klabu ya TP Mazembe ya Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Mbwana Samatta zinazidi kuchukua nafasi. Samatta ambaye anatajwa kukaribia kujiunga na klabu ya KRC Genk ya Ubelgiji bado hajasaini mkataba na klabu hiyo licha ya yeye na Genk kukubaliana maslahi binafsi.
January 4 stori ya Samatta na Genk imerudi kwenye headlines kwa mara nyingine tena, kikubwa kinachochelewesha uhamisho wa Samatta kwenda KRC Genk ni klabu yake ya TP Mazembe ambayo bado ina mkataba na Samatta wa miezi mitatu, hivyo wanataka kumuuza kwa dau kubwa, licha ya kuwa mkataba wake umekaribia kumalizika.
TP Mazembe wanasita kumuuza Samatta kwa Euro 550000 ambazo ni zaidi ya bilioni 1.2 za Tanzania, hivyo wanatajwa kumtuma mtu wao kuja Dar Es Salaam na kumshawishi Samatta aongeze mkataba hadi December 30 2016, kitendo ambacho kingewalegeza KRC Genk na kutoa fedha nyingi zaidi ili wamsajili.
Hata hivyo ujanja wa TP Mazembe kumshawishi Samatta afanye hivyo haukuungwa mkono na meneja wake na familia yake. Taarifa mpya ni kuwa January 3 mmiliki wa TP Mazembe Moise Katumbi alifanya mazungumzo ya saa moja kwa njia ya simu na CEO wa KRC Genk na mambo yamekaa vizuri.
CHANZO CHA STORI HII: shaffihdauda.com
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyezahapa>>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.