Bado headlines za mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania anayekipiga katika klabu ya TP Mazembe ya Jamuhuri ya Kidemokrasi ya Kongo Mbwana Samatta zinazidi kuandikwa kila siku. Kwa sasa Mbwana Samatta anakaribia kujiunga na klabu ya KRC Genk ya Ubelgiji kwani kinachosubiriwa kwa sasa ni kuafikiana na ada ya uhamisho wa mshambuliaji huyo.
Klabu ya TP Mazembe ambayo ndio inayomilikiwa na Moise Katumbi inahitaji dau la euro milioni 2.5 ambazo ni zaidi ya bilioni 6 za kitanzania kama ada ya uhamisho wa nyota huyo aliyebakiza mkataba wa miezi minne wa kuendelea kuitumikia timu hiyo, ila kwa upande wa Simba wao wanafaraja na kuuzwa kwa Samatta kwenda Genk, kwani itavuta mkwanja kutoka katika dau la Samatta.
Kama TP Mazembe watafanikiwa kumuuza Samatta kwa zaidi Tsh Bilioni 6 kwenda KRC Genk, klabu ya Simba itafanikiwa kuvuna Tsh bilioni 1.2 kama ada sehemu ya makubaliano yaliyomo katika mkataba wa mauzo ya Mbwana Samatta aliyeuzwa mwaka 2011 kwenda TP Mazembe akitokea Simba. Mkataba wa mauzo ya Samatta ulikuwa na makubaliano kama TP Mazembe watamuuza Samatta nje ya klabu yao, basi Simba itapata asilimia 20 ya ada ya uhamisho.
CHANZO: boiplus.blogspot.com
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyezahapa>>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.