Kwa mara ya kwanza klabu ya KRC Genk ya Ubelgiji ambayo inaongozwa na kocha lakini inachezewa na nahodha wa timu ya taifa ya Tanzania Mbwana Ally Samatta, imempa nafasi ya kuanza katika mchezo wa leo dhidi ya klabu ya KV Oastende.
Samatta amepata nafasi hiyo ya kuanza mchezo wa leo March 13, ikiwa ni zaidi ya mechi nne amekuwa akiichezea timu hiyo akitokea benchi. Baada ya Samatta kuanza first eleven, alipachika goli la kwanza kwa timu yake dakika ya 25 ya mchezo, lakini hilo pia ni goli lake la pili toka ajiunge na KRC Genk.
Goli la Samatta lilifuatiwa na neema kwa KRC Genk, kuibuka na ushidi wa goli 4-1, magoli ya KRC Genk yalifungwa na Mbwana Samatta dakika ya 25, Balley dakika ya 39, Pozuelo dakika ya 81 na Camargo dakika ya 88, wakati goli la kufutia machozi kwa KV Oostende lilifungwa na Siani dakika ya 90.
Video ya goli la Samatta
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana naMillardAyo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE