Bado furaha ya watanzania kumuona Mbwana Samatta akicheza soka Ulaya ipo moyoni mwao, baada ya kumuona kwa mara ya kwanza akiichezea klabu yake ya KRC Genk kwa dakika 17 February 6 katika mchezo dhidi ya Mouscron FC, huku mchezo ukimalizika kwa KRC Genk kuibuka na ushindi wa goli 1-0 ugenini.
Klabu ya KRC Genk inarudi jijini Genk kucheza mchezo wake wa Ligi katika uwanja wake wa nyumbani Cristal Arena Jumamosi ya February 13 kucheza mechi yao 26 ya Ligi dhidi ya Beveren W iliyopo nafasi ya 13 katika Ligi ikiwa na point 26 wakati KRC Genk ya Samatta ipo nafasi ya 5 ikiwa na point 38.
Huenda Mbwana Samatta akapata nafasi ya kucheza mechi ya Jumamosi dhidi ya Beveren W na kuweka rekodi ya kucheza mechi yake ya pili akiwa na KRC Genk lakini pia akicheza mechi ya kwanza ya mashindano katika uwanja wa nyumbani wa KRC Genk kama mchezaji rasmi wa klabu hiyo.
Uwanja wa Cristal Arena unaotumiwa na KRC Genk kama uwanja wa nyumbani, ulijengwa mwaka 1999, una uwezo wa kuchukua zaidi ya mashabiki 20000, unatumika kwa michezo mingi, ila kwa kiasi kikubwa mchezo wa mpira wa miguu ndio huchezwa sana, kabla ya kuanza kwa msimu wa 2008/2009 uwanja huo ulikuwa unaitwa “Fenixstadion” ila mwaka 2007 KRC Genk walisaini mkataba na kampuni ya bia ya Alken-Maes ili kukodisha jina.
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwapia ungana na MillardAyo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyezahapa>>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.