Maonesho ya aina yake ya SAMIA Kilimo Biashara yameanza Jana Wilayani Gairo huku yakihudhuriwa na maelfu ya Wananchi walioshiriki ili kupata huduma mbalimbali kutoka kwa wadau wa Sekta ya Kilimo, Mifugo na Mazingira.
Maonesho haya yanalenga kutekeleza Mkakati wa Kitaifa ulioasisiwa na Serikali ya awamu ya Sita chini ya Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan wa Ajenda10/30 wenye lengo la kukuza Sekta ya Kilimo (Mazao na Mifugo) kama njenzo ya kuinua uchumia wa Wilaya ya Gairo, kukuza kipato Cha mwananchi mmoja mmoja na kupambana na umasikini.
Maonesho haya ya Siku 7 yamebeba Ajenda Kuu 5 ambazo ni Ushiriki wa Wananchi kwenye Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024, Nishati Safi ya Kupikia na Fursa ya Biashara ya Kaboni, Ushirika na Mifumo ya Kielekroniki ya Uuzaji wa Mazao (Mfumo wa Stakabadhi za Ghala), Kilimo na Ufugaji wa Kibiashara, Lishe na Hifadhi ya Jamii (Bima ya Afya kwa Wote na Hifadhi ya Jamii kwa wakulima na wafugaji).