Rais Samia Suluhu Hassan amesema uwekezaji katika Bandari ya Dar es Salaam utaifanya iwe na uwezo mkubwa na ufanisi zaidi wa kuhudumia wateja wake kutoka popote duniani.
Rais ameyasema hayo kwenye hotuba yake kama mgeni rasmi wa maadhimisho ya miaka 59 ya Uhuru wa Zambia iliyofanyika Ikulu ya Lusaka, Zambia.
Rais aliitumia nafasi hiyo kushawishi serikali na wafanyabiashara wa Zambia kuendelea kuitumia Bandari ya Dar kama kituo chake Kikuu cha usafirishaji na upasuaji wa mizigo yake.