Aliyekuwa rais wa Zambia Michael Sata amefariki usiku wa jana tarehe 28 Oktoba kutokana na ugonjwa ambao bado serikali ya nchi hiyo haijaweka wazi.
Sata (77) amefariki akiwa anatibiwa nchini Uingereza alikokuwa amelazwa kwa zaidi ya mwezi mmoja.
Rais huyo amefariki siku 4 baada ya nchi hiyo kusherehekea madhimisho ya miaka 50 tangu ipate uhuru, ambapo kutokana na kuwepo nje ya nchi akipata matibabu hakuhudhuria sherehe za maadhimisho hayo.
Rais Sata ambaye amekuwa maarufu kwa jina la ‘King Cobra‘ amekaa madarakani kwa takribani miaka 3 tangu achaguliwe kushika wadhifa huo mwaka 2011, ambapo anakuwa rais wa 2 kufariki akiwa madarakani nchini humo baada ya Levy Mwanawasa, aliyefariki mwaka 2008.