Hekaheka ya leo July 26, 2017 imetokea Kimara DSM ambako mwanaume mmoja adaiwa kumchoma kisu aliyekuwa mkewe kufuatia kumkatalia kurudiana naye baada ya kumuacha kwa talaka tatu.
Tukio hilo linadaiwa kutokea wakati ambapo mwanaume huyo kwenda kwa mwananmke na kumwambia kuwa anataka warudiane lakini mwanamke alimkatalia kwa kuwa alishajijenga na maisha yake. Kwa jibu hilo mwanaume akaamua kumchoma kisu mwanamke huyo katika sehemu mbalimbali za mwili na kumsababishia majeraha.
Kutokana maumivu, mwanamke huyo alipiga kelele za kuomba msaada ambapo aliokolewa na mama yake mzazi na majirani ambao walimuwahisha Hospitali ya Mwananyamala kwa ajili ya matibabu huku mwanaume akikimbia kusikojulikana.
FULL STORI nimekuwekea hapa…bonyeza PLAY kutazama…
HEKAHEKA: Mwanamke adaiwa kumkata sehemu za siri mtoto wa jirani yake…kisa?