Saudi Arabia imetoa wito wa kusitishwa mara moja mapigano huko Gaza, na kuitaka jumuiya ya kimataifa kuongeza uungaji mkono kwa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi wa Kipalestina UNRWA.
Mwakilishi wa Kudumu wa Saudi Arabia katika Umoja wa Mataifa, Balozi Abdulaziz Al Wasil, alilaani “matumizi mabaya ya kura ya turufu” na matumizi ya kuchagua ya sheria za kimataifa, akisema kuwa mambo hayo yamechangia kuendelea kwa “vita vya mauaji ya halaiki” ya Israel na kupanuka kwa Israel na uhalifu huko Gaza.
Aidha amesisitiza kuwa ukosefu wa uwajibikaji umezidisha tu mateso ya wananchi wa Palestina.
Mauaji ya kimbari ya Israel huko Gaza sasa katika siku yake ya 434 yamesababisha vifo vya Wapalestina 44,835 na wengine 106,356 kujeruhiwa.
Nchini Lebanon, Israel imewauwa watu 4,047 tangu Oktoba 2023 na inaendelea kukiuka makubaliano ya mapatano ya Novemba 27.