Saudi Arabia inalaani uvamizi wa Israel katika hospitali ya Shifa katika mji wa Gaza, na kuuita “ukiukaji wa wazi wa sheria za kimataifa” katika taarifa kutoka kwa Wizara ya Mambo ya Nje.
Pia imelaani kile ilichosema ni shambulizi karibu na hospitali nyingine na kutoa wito kwa mashirika ya kimataifa kuiwajibisha Israel.
Israel inasema wanajeshi wake wanafanya operesheni iliyolengwa huko Shifa, ambapo kwa muda mrefu imekuwa ikiishutumu Hamas kwa kudumisha kituo cha amri cha chinichini – madai yanayoungwa mkono na Marekani. Hamas na wafanyikazi wa hospitali wamekanusha madai hayo.
Vikosi vya Israel vinavyosaka eneo la matibabu tangu jana vinasema kuwa wamepata bunduki na dalili nyingine kuwa magaidi wa Hamas walikuwa ndani, lakini hawajaonyesha ushahidi wowote kuhusiana na kituo hicho kinachodaiwa kuwa kama kamandi.
Kabla ya vita hivyo, Saudi Arabia ilikuwa katika mazungumzo na Marekani kuhusu uwezekano wa kurejesha uhusiano wa kawaida na Israel.