Mtoto anaweza kuonesha mapenzi yake waziwazi kwa njia yoyote ile japo mara nyingine kwa njia ambayo inakutia hasara ila ndio hivyo mtoto kaamua kukuonesha hivyohivyo upendo wake !!
Siku ya akina baba duniani imepita, nimekipata hiki kisa kingine ambacho kimechukua headlines mitandaoni… mtoto kachukua screwdriver alafu kachora kwenye gari ya baba yake >>> “Nampenda baba yangu (I love my dad)“>>> picha imechukua headlines mitandaoni lakini bado haijafahamika jina la mtoto huyo wala nchi ambako ishu hii imetokea.
Mtoto hata hajawaza yani kwamba hiki alichokifanya itabidi baba yake arudi gereji ili hiyo gari ipigwe rangi upya… Unaikuta gari yako mtoto kaifanya hivi unafanyaje mtu wangu?