Leo February 9, 2018 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dr. Mwigulu Nchemba amelitaka Jeshi la Polisi nchini kuziachia pikipiki ambazo wamezishikilia kwa muda mrefu na zina makosa madogo na kwamba wasikae nazo kwa muda mrefu mpaka zikawa vyuma chakavu.
Dr. Mwigulu amesema zile yenye makosa makubwa kama uhalifu wa kivita, dawa ya kulevya wabaki nazo na wafanye utaratibu wa kuwapeleka Mahakamani au kuziteketeza na zenye makosa madogo wazirudishe kwa wamiliki na kuwapa elimu wamekosea wapi.
“Wapeni masomo wamekosea wapi, waelekezeni na waliowabishi warekebisheni lakini tusirundike tukatengeza vyuma chakavu kwa hivi vitu ambavyo utatuzi wake tunao, tutumie huu mkono kwa kutatua yale ambayo yapo ndani ya mamlaka yetu” – Dr Mwigulu
Amesema kuwa ipo haja sasa vijana kufundishwa zaidi kuhusu sheria za usalama barabarani ili kupunguza ajali za pikipiki na mlundikano wa pikipiki katika vituo vya polisi nchini kwani kila anapopita katika vituo vya polisi hukuta pikipiki nyingi na makosa yao ni madogomadogo.
Mamlaka ya TWAKIMU ‘Hali ya mfumuko wa Bei mwezi January’
Wema Sepetu baada ya kutoka Mahakamani