Kamati ya Maudhui imeundwa chini ya kifungu 26 (I) cha Sheria ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania ya 2003. Kamati hii huteuliwa na Waziri mwenye dhamana ya mambo ya utangazaji.
Kamati hii inasikiliza malalamiko yanayohusiana na maudhui ya utangazaji.
Pamoja na utaratibu huu, malalamiko yanayohusiana na maudhui pia yanafuata hatua nne zilizoainishwa hapo juu.
Pamoja na utaratibu wa kuwasilisha malalamiko kuhusiana na huduma na bidhaa za mawasiliano,
watumiaji/walaji wana haki nyingine za kuwasilisha malalamiko yao kwenye vyombo vingine vya
kutoa haki baada ya kukamilika kwa utaratibu wa kulalamika pale ambapo suala litakalolalamikiwa
halihusu huduma au bidhaa za mawasiliano.