Leo March 21, 2019 Nakusogezea stori inayohusiana na tamko lililotolewa na BOT na leo Azania Bank wamelikamilisha ambapo wamewahakikishia wateja wake kuwa itaendelea kutoa huduma za ubora wa hali ya juu kama ambavyo imekuwa ikifanya kwa kipindi kirefu sasa.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Azania, Charles Jackson Itembe ameyasema hayo leo jijini DSM wakati akizungumza na wanahabari. Hii ni baada ya Benki kuu ya Tanzania (BoT)
kutoa tamko kuhusiana na kukamilika rasmi kwa mchakato wa kuhamishia Mali na Madeni ya
iliyokuwa Benki M na kuzihamishia benki ya Azania.
“Tumeingia kwenye makubaliano na BoT ya kuinunua benki M ya DSM hatua ambayo
itapanua soko letu katika sekta ya kifedha hapa nchini Tanzania. Ununuzi huu wa benki M unatarajiwa kuongeza ufanisi kupitia michakato iliyoboreshwa, utamaduni na kuongeza soko”. Itembe
Mnamo Agosti 2018, BOT iliiweka benki M chini ya uangalizi maalum kutokana na beki hiyo
kushindwa kutoa huduma za kifedha kwa mujibu wa sheria inayosimamia mabenki.
Ununuzi huu umefanikiwa baada ya benki ya Azania kutuma maombi na andiko kwenda BOT juu
ya nia yake ya kuinunua Benki M, baada ya hapo majadiliano marefu baina ya wanahisa na Benki
Kuu yaliendelea kwa miezi kadhaa.
Benki ya Azania kupitia kwa wanahisa wake wakubwa ambao ni PSSSF (51.95%), NSSF(27.99%), EADB(0.51%),Wanahisa wadogo (0.34%) pamoja na wanahisa wapya (National Health Insurance Fund(17.42%) na Workers Compensation Fund (1.79%)) hatimae kufikia muafaka wa upatikanaji wa mtaji na ukwasi wa uendeshaji wa benki baada ya kuichukua Benki M.
Itembe amesema aina hii ya ununuzi wa benki inajulikana kama “sheria ya uchukuzi wa
kiutendaji”
‘’Tuliona ununuzi wa benki hii ni muhimu kwa utendaji za benki ya ABL. Ukamilisho wa uambatanisho wa benki hizi mbili unatarajiwa kukamilika siku 45 kwanzia siku tulio ingia katika makubaliano ya mkataba wa ununuzi na BOT (Ijumaa, 15.03.2019).” Itembe
“Tutatangaza rasmi siku ya ufunguzi wa tawi amabalo wateja wetu w Benki M wataendelea kupokea huduma bora kufikia matarajio yao kupitia mtandao na matawi ya Benki ya Azania na matawi matatu amabayo awali yalikuwa wakimilikiwa na Benki M.’’ Itembe
Uamuzi wa kupewa taasisi hiyo ulifanywa katika mkutano wa mwaka ulifanyika Desemba 21,2018 ambapo wanahisa walikubaliana kuongezea mtaji Benki ya Azania na kukaribisha wanahisa wapya ambao nao pia walikubali kuongeza mtaji iliyofanya Azania kuwa imara na kuweza kuipata Benki M.
Uchukuzi huu umeipeleka Azania mbali zaidi kuongeza idadi ya matawi kutoka 19 hadi 22 na kuongeza mtaji wake kutoka billion 64 za kitanzania mpaka billion 181 za kitanzania wakati jeduwali la mizani kuvuka trilioni kutoka awali ambapo ilikuwa nusu trilioni.
“Baada ya kipindi hiki cha siku 45 tunatarajia kufungua milango kwa wateja wote wa Benki M ambao watahudumiwa katika tawi lolote la ABL watakalopendelea nchini Tanzania. Pia mchakato huu utapelekea kubadili mwonekano wa matawi ya benki M ya Kisutu, Pugu na Arusha ili yafanane na yale ya benki ya Azania” Itembe.
Kwa mujibu wa Itembe, hatua hii mpya inaifanya ABL kuwa (Tier One bank) kwa namna yoyote
ile haitabadilisha muundo wa utendaji kazi wa benki badala yake utaunganisha mifumo hii
miwili.
“Kama sehemu ya uendeshaji, Benki ya Azania itaendelea na utekelezaji wa mikakati yake yakisera ya miaka mitano (Five-Year strategic plan) ambayo itafanyiwa maboresho ili kuendana na huu Muunganiko wa Benki hizi mbili. Lengo letu kubwa ni kuhakikisha wateja wa iliyokuwa Bank M wanaendelea kupata huduma zilizo bora zaidi”–Itembe
FULL HD: BOT ILIVYOTANGAZA KUHAMISHA MALI NA MADENI YA BANK M