Leo January 22, 2018 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. John Magufuli amepokea hati za utambulisho kutoka kwa Mabalozi 6 walioteuliwa kuziwakilisha nchi zao hapa nchini.
Mabalozi waliowasilisha hati zao ni Konstantinos Moatsos ambaye anatokea Ugiriki mwenye makazi yake Nairobi nchini Kenya, Fafre Camara, Balozi wa Mali mwenye makazi yake Addis Ababa Ethiopia na Dina Mufti Sid ambaye ni Balozi wa Ethiopia hapa nchini mwenye makazi yake Nairobi Kenya.
Wengine ni Elizabeth Taylor yeye ni Balozi wa Colombia nchini Tanzania makazi Nairobi Kenya, Martin Gomez Bustillo, Balozi wa Argentina hapa nchini ambaye makazi yake ni Nairobi Kenya na Uriel Norman R. Garibay ambaye yeye ni Balozi wa Ufilipino makazi yake Nairobi nchini Kenya.
Rais Magufuli amewapongeza Mabalozi wote kwa kuteuliwa kuziwakilisha nchi zao hapa nchini na ameahidi kuwapa ushirikiano utakaowezesha uhusiano na ushirikiano kati ya Tanzania na nchi zao kukua zaidi.
Pia amewahakikishia kuwa Tanzania inatambua uwepo wa fursa mbalimbali za kibiashara na kiuchumi katika nchi zao pamoja na ujuzi na uzoefu katika nyanja mbalimbali, na kwamba ni matarajio yake kuwa ujio wao utasaidia kuongeza manufaa ya kiuchumi na kubadilishana uzoefu.
BREAKING: Said amwaga machozi baada ya Scorpion kuhukumiwa miaka 7
“Hata kama wewe ni upinzani, chagua CCM sasa hivi sababu….. ” – MWIGULU