Matukio mbalimbali yanayohusishwa na ‘kuapishwa’ kwa Kiongozi wa Upinzani NASA Raila Odinga yanaendelea kuripotiwa ambapo jingine ni la mwanaume mmoja kutimiza ahadi yake ya kunyoa rasta zake endapo Raila atafanikiwa kuapishwa.
Mwanaume huyo David Oguyo ambaye amefuga rasta zake kwa zaidi ya miaka 10 alisema atazinyoa Raila akiapishwa ikiwa ni ishara ya kufurahishwa kwake na jambo hilo na jana alitimiza ahadi hiyo kwa kwenda saloon na kunyoa.
Oguyo ambaye ni baba wa watoto sita ameieleza Citizen Digital kuwa aliweka nadhiri hiyo tangu uchaguzi wa mwaka 2007 na kukata rasta zake pia ni ishara ya kuamini kuwa maisha bora kwa wananchi yanakuja.
Alichokifanya Lukuvi kabla ya kuondoka Mwanza