Aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje, Bernad Membe amefunguka kwamba atamtafuta rafiki yake ambaye ni mfanyabiashara Rostam Aziz ili kumshauri azungumzie masuala ya Kiuchumi kwa kuwa wote wamekatwa mikia.
Membe ameyasema hayo mbele ya waandishi wa habari baada ya kuwepo kwa maneno kwamba Rostam amemtaka atulie na aachane na mambo ya kutaka kugombea urais.