Kutoka vyombo vya habari ya kimataifa leo March 28, 2018 ameonekana kijana mmoja ajulikanaye kwa jina la Daniel Hold wa nchini Uingereza ambaye anasumbuliwa na tatizo la kupooza kwa ubongo lakini anasema suala hilo halitamzuia kufikia malengo yake.
Daniel amehojiwa na CNN na kueleza kuwa ana degree ya sheria na watu wengi wamekuwa wakisita kumuajiri ili awafanyie kazi zao kutokana na hali yake lakini hatokata tamaa.
Kutokana na ugonjwa huo, Daniel amepoteza uwezo wake wa kuzungumza vizuri kama mtu asiye na maradhi hayo, jambo linalofanya watu wasite kumchukua kama mwakilishi wao kwenye kesi mahakamani kwa kuhofia kushindwa.
Daniel anasema lengo lake ni kuja kuwa Wakili atakayeruhusiwa kuwawakilisha watu kwenye mahakama za juu nchini humo.
“Wananchi wanashangilia bila kujua lile ni bomu” – Mwenyekiti CCM Mtwara