Mkazi mmoja kutokea Mbweni jijini Dar es Salaam, Irene Mbuya (18), amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni akikabiliwa na kosa la kuiba mtoto jinsia ya kiume aitwaye (Paul Ibrahim -miaka(2).
Mbele ya Hakimu Anipha Mwingira, Wakili wa Serikali Ramadhan Mkimbu, alidai kuwa mtuhumiwa alitenda kosa hilo January 30, 2018 eneo la Tegeta.
Inadaiwa mtuhumiwa huyo alikuwa na nia ya kuwanyima umiliki halali wa wazazi wa mtoto huyo wakati akitambua ni kinyume cha sheria za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Baada ya kusomewa maelezo hayo Mtuhumiwa alikanusha kutenda kosa hilo ambapo upande wa Jamhuri uliomba tarehe nyingine ya kumsomea hoja za awali kwa kuwa upelelezi umekamilika.
Hakimu Mwingira alidai kwamba shtaka hilo linadhaminika kwa mujibu wa sheria hivyo alimtaka kuleta wadhamini wawili waaminifu.
“Dhamana yako iko wazi hivyo kila mdhamini anatakiwa alete barua za utambulisho wanapoishi, vitambulisho vyao pamoja na kuwekea bondi ya maandishi shilingi laki tano,” -Hakimu Anipha Mwingira.
Hata hivyo, mtuhumiwa alishindwa kutimiza masharti ya dhamana alirejeshwa Mahabusu na kesi hiyo imeahirishwa hadi Februari 27, 2018 kwa ajili ya mshtakiwa kusomewa maelezo ya awali (PH).
Kamanda Mpinga ametaja Waliokamatwa na Meno ya Tembo yenye Thamani ya Milioni 33