Leo Mei 8, 2019 Mkurugenzi wa Mashitaka Nchini (DPP) Biswalo Mganga ambapo amezungumzia utekelezwaji wa amri ya Mahakama Kuu ya Tanzania kuhusu kutaifishwa mali za Kampuni ya Development Enterpreneuship for Community Initiative (DECI) ikiwemo Sh.Bilioni 14.3.
DPP Mganga amezungumzia hilo mbele ya waandishi wa habari ambapo amesema anawatahadharisha Mameneja wa benki kutojaribu kuhamisha wala kuchukua fedha hizo ambazo ni Bil.14.3 zilizotaifishwa Mahakama zilizopo katika matawi yao.