Kutokea nyumbani kwa marehemu Dr.Reginald Mengi, Mwanasheria wa familia hiyo Michael Ngalo amesema mwili wa Dr.Mengi utawasili nchini Mei 5, 2019 saa 8:30 mchana.
Ngalo amesema mara baada ya mwili kuwasili utapelekwa Hospitali ya Lugalo na Mei 6, utapelekwa viwanja vya Karimjee kwa ajili ya kuagwa kisha kurejeshwa nyumbani kwake kwa ajili ya maombi.
“Baada ya hapo Mei 7, mwili utasafirishwa kwenda Moshi na utazikwa Alhamis asubuhi ya Mei 8, 2019,“amesema.