Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESBL) imeanzisha kampeni maalumu kwa ajili ya kutoa elimu kwa wanafunzi wa Kidato cha 5 na 6 katika shule mbalimbali za sekondari kwa lengo la kuwaelimisha wakati wa kuombaji mikopo kupitia Internet Cafe.
Akizungumza hatua hiyo, Mkurugenzi Msaidizi Utoaji Mikopo HESBL Sarah Fihavango amesema wanapita katika shule za sekondari na kuwaelimisha juu ya ujazaji fomu za mikopo ambapo wamegundua wengi wanakosea kujaza na kukosa mikopo.
“Hatutaweza kuppita shule zote Tanzania isipokuwa tunapita katika shule chache ambazo wengine watakuwa mabalozi, pia wengi wanajisahahu kwa kuwaachia watu wa Internet Cafe kujaza fomu zao za mikopo,” amesema.