Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango amezitaka sekta za kifedha kutumia kongamano la 21 la wadau sekta hiyo kuja na hatua za muda mfupi zitakazosaidia kukabiliana na uhaba wa fedha za kigeni nchini.
Makamu wa Rais Dkt.Philip Mpango ametoa kauli hiyo katika ufunguzi wa kongamano la 21 la wadau wa sekta ya Fedha ulioambatana na ufunguzi wa mfumo wa Taifa wa malipo ya papo kwa papo (TIPS) ambapo amesisitiza washiriki hao kujadili na kuja muafaka wa changamoto ya uchache wa fedha za kigeni unaothiri ustawi wa sekta nyingine.
“Ninawaomba washiriki wa kongamano hiki kutafakari kwa kina changamoto ya uhaba wa fedha za fedha za kigeni iliyopo hivi sasa “
Kwa upande wake Gavana wa benki kuu Tanzania Emmanuel Tutuba ameeleza kuwa kuasisiwa kwa mfumo huo kieletroniki kutachochea hatua ya mapinduzi katika sekta za kifedha kwa kuokoa muda na ghalama.