Rais wa Senegal Macky Sall ametangaza siku ya Jumatatu, katikati ya mgogoro mkubwa kuhusiana na kuahirishwa kwa uchaguzi wa urais, muswada wa msamaha wa jumla unaohusishwa na machafuko yaliyoikumba nchi yake tangu mwaka 2021.
“Kwa matumaini ya maridhiano ya kitaifa, nitawasilisha kwa Bunge siku ya Jumatano katika kikao cha Baraza la Mawaziri muswada wa jumla wa msamaha kuhusu vitendo vinavyohusiana na maandamano ya kisiasa yaliyotokea kati ya mwaka 2021 na 2024,” rais Sall amesema kwa kufungua mashauriano huko Diamniadio karibu na Dakar, kujaribu kupata makubaliano juu ya tarehe ya uchaguzi wa urais.
“Hii itasaidia kutuliza mvutano wa kisiasa na kuimarisha zaidi uwiano wetu wa kitaifa,” amesema. Amebainisha nia yake ya kuandaa uchaguzi wa urais ifikapo Juni-Julai, huku kundi kubwa la upinzani likidai uchaguzi kufanyika kabla ya Aprili 2.
Nia yangu na na matakwa yangu makuu ni kufanya uchaguzi wa urais haraka iwezekanavyo na kabla ya msimu wa baridi ujao (msimu wa mvua), na kwa amani,” ali
ame, huku akitangaza kuondoka mamlakani wakati tu muhula wake utakapo tamatika Aprili 2.