Kufungwa kwa internet, kupigwa marufuku kwa Tik Tok pamoja na kukamatwa kwa wanahabari ni miongoni mwa hatua zinazoonyesha kushuka kwa uhuru wa habari nchini Senegal, taifa ambalo wakati mmoja lilikuwa mfano mwema wa demokrasia.
Wanaharakati wa uhuru wa habari pamoja na wanahabari wanaofanya kazi kwenye taifa hilo la Afrika Magharibi wanasema kwamba kushuka kwa haki hizo kunafanyika wakati wa maandamano makubwa kufuatia kukamatwa kwa kiongozi mashuhuri wa upinzani, kabla ya kufanyika kwa uchaguzi mkuu mapema 2024.
Mkurugenzi wa shirikia la wanahabari wasio na mipaka tawi la Afrika magharibi Sadibou Marong wakati akizungumza na VOA amesema, “Wakati mmoja Senegal ilikiwa kielelezo cha uhuru wa habari lakini hadhi yake imeshuka kutokana na hatua kadhaa, moja wapo kuu ikiwa ni vitisho na matusi kutoka kwa wanasiasa.