Nchini Senegal, chama cha PASTEF kimetangaza hivi punde Jumapili usiku Novemba 19 mpango wake B kwa uchaguzi wa urais wa Februari 2024, baada ya kushindwa kwa kiongozi wake Ousmane Sonko, ambaye alishindwa kusajiliwa tena.
Chama cha upinzani kimemteua Bassirou Diomaye Faye, katibu mkuu na mshirika wa karibu wa Ousmane Sonko kuwa mgombea wake.
“Kumfadhili Diomaye Faye ni kumfadhili Sonko”: hii hapa ni kauli mbiu mpya ya chama cha PASTEF ambacho kinazindua kampeni ya ufadhili chini ya wiki tatu kabla ya tarehe ya mwisho.
Kutkokana na mamlaka kukataa kumpa Ousmane Sonko fomu zake za ufadhili, chaguo lilimwangukia Bassirou Diomaye Faye, ambaye ni mpango B wa chama. Haya kulingana na taarifa iliyochapishwa na wagombea wengine wanne wa PASTEF kwania kiti cha urais, “hatu iliyoidhinishwa” na Ousmane Sonko, ambaye kwa sasa yuko gerezani.
Katibu mkuu wa PASTEF na mshirika wa karibu wa Ousmane Sonko yuko kizuizini tangu mwezi Aprili. Diomaye Faye alikamatwa baada ya kuchapisha chapisho kwenye mitandao ambapo alikosoa tabia ya baadhi ya majaji katika kesi ya kashfa kati ya Ousmane Sonko na Waziri wa Utalii Mame Mbaye Niang.
Chama kinatoa wito kwa wafuasi wake kukiunga mkono kwa wingi – njia ya kutaka kuonyesha uzito wa kisiasa wa harakati na uwezo wake wa kuhamasisha.