Ni Agosti 24, 2023 ambapo Afisa Habari wa Klabu ya Young Africans, amezungumza na vyombo vya habari kuhusu mchezo wa Marudio dhidi ya ASAS FC Djibouti utakaochezwa Jumamosi hii kwenye Uwanja Azam Complex Chamazi saa kumi na moja jioni.
“Niko hapa mbele yenu kuwakaribisha Wanachama, Mashabiki na Wapenzi wa Young Africans kwenye mchezo wetu wa marudiano #CAFCL dhidi ya Asas Djibouti Jumamosi ya tarehe 26.08.2023 Azam Complex, Chamazi saa 11:00 Jioni”– Alikamwe
Malengo yetu msimu huu Kimataifa ni kuhakikisha tunatinga hatua ya makundi ya ligi ya mabingwa barani AFRIKA, mashindano ambayo hatujashiriki kwa muda mrefu, tumeshafanya vizuri kwenye mashindano ya shirikisho na sasa malengo yetu ni kufanya vizuri kwenye ligi ya mabingwa”- Alikamwe
“Mechi dhidi ya Asas bado haijaisha kama ambavyo watu wengi wanadhani, michezo hii ya Kimataifa inahitaji umakini sana ili uweze kwenda kwenye hatua inayofata na sisi hatuwezi kumdharau mpinzani yoyote yule hata kama tumefunga mchezo wa awali– Alikamwe
“Viiingilio vya mchezo wetu wa Jumamosi dhidi ya Asas Djibouti Mzunguko -5,000
VIP B – 20,000
VIP A – 30,000
Mechi zetu msimu huu mashabiki watakuja kwa wingi kwa sababu wanakuja kutazama burudani ya kipekee, hivyo ukichelewa kukata tiketi, unajiweka kwenye purukushani ambazo hazina ulazima’- Alikamwe
Tahadhari
Kumekuwa na malalamiko mengi kwa baadhi ya mashabiki kushindwa kuingia Uwanjani ingawa wana tiketi. Kwa utafiti mdogo tumegundua kuwa mashabiki wengi wanauziwa tiketi feki napenda kuwaomba Mashabiki wetu wanunue tiketi na kuwahi Uwanjani mapema ili kuepuka changamoto na usumbufu wa kukosa tiketi getini siku ya mechi”- AliKamwe