Baada ya picha ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan kuonekana katika jengo refu maarufu duniani la Burj Khalifa Dubai.
Sasa imeibuka maswali mengi sasa hapa tunaen msemaji wa Serikali Gerson Msigwa ambae ametolelea ufanunuzi.
“Serikali haijalipia kuweka tangazo la Tanzania katika jengo refu kuliko yote Duniani liitwalo Burj Khalifa lililopo katika Jiji la Dubai, tangazo hilo limewekwa kwa lengo la kuitangaza Tanzania kutokana na uhusiano mzuri uliopo kati ya Nchi yetu na Umoja wa Falme za Kiarabu”
“Utawala wa Dubai umeweka tangazo hilo kwa kutambua ziara ambayo Rais Samia Suluhu Hassan ameifanya Dubai na umeahidi kuendelea kuitangaza Tanzania kupitia jengo hilo maarufu” ——— Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa
TAZAMA JENGO REFU ZAIDI DUNIANI DUBAI, LIKIWA NA PICHA YA RAIS WA TANZANIA SAMIA SULUHU HASSAN