Serikali imesema kuwa inaendelea na jitihada za kuhakikisha inatoa fursa mbalimbali za mikopo na fursa za ujasiriamali kwa watanzania walio na umri wa zaidi ya miaka 35 ili kuwezesha kupata fedha kutoka kwenye mabenki na mifuko maalum iliyopewa vibali vya ukopeshaji.
Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano Tanzania Kassim Majaliwa ameyasema hayo wakati akijibu swali la Mbunge wa jimbo la Ushetu Emmanuel Cherehani ambaye aliuliza juu ya mikopo inayotolewa kwa vijana, wanawake na makundi maalum isiyohusisha watanzania walio na zaidi ya miaka 35 ambao ndio wategemezi wa familia.
“Serikali haijalisahau kundi la watanzania walio na zaidi ya miaka 35 na inafanya jitihada za kuzungumza na mabenki na mifuko maalum ya ukopeshaji ili kutoa fursa kwa kundi hili kuendeleza shughuli zao za ujasiriamali” Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.