Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli amewataka viongozi wa Serikali na wale ambao watateuliwa kuwa Marais siku zijazo, wahakikishe hawafanyi ubinafsishaji wowote wa mashirika badala yake yabaki kuwa chini ya serikali ili yaweze kuendelea kutoa huduma kwa wananchi.
“Niwaombe viongozi wenzangu serikalini hili liwe fundisho tusikubali tena kubinafsisha vitu vya msingi katika nchi, tulibinafsisha ndege na treni tukaja kuanza upya, mimi sitakuwa Rais wa maisha lakini natoa ujumbe kwa wale watakaokuja baadaye hili liwe fundisho” JPM
“Hata nchi zilizoendelea mashirika yao hawajayabinafsisha, ibaki kuwa ndani ya serikali na inapokuwa ndani ya seriklai huduma kwa wananchi wanyonge itawafikia” JPM
“Vichwa vya Watanzania vina akili mno lakini tatizo hatuaminiani, ninawaomba kupitia mfano huu wa TRC tuanze kujiamini tutafanya makubwa ambayo wengine hawawezi kuyafanya, mabehewa yote ya mizigo 347 yamekarabatiwa hapa, na 20 ya abiria nayo yamekarabatiwa hapa” JPM